Kufuatia mchakato wa kuomba marekebisho ya bei za maji uliofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Chalinze (CHALIWASA) Mwezi Agosti 2018. Uongozi wa CHALIWASA unapenda kuwajulisha wateja wake kuwa, Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeidhinisha bei mpya za huduma za Maji Safi, Munganisho Mapya ya Maji Safi (New Connection), kurejesha huduma ya maji (Reconnection fee), Boza Maji Safi na Maji Taka kama zinavyoonekana katika majedwali yafuatayo kuanzia tarehe 01 Juni 2019:-